Exodus 29:4-9

4 aKisha mlete Haruni na wanawe kwenye lango la Hema la Kukutania na uwaoshe kwa maji. 5 bChukua yale mavazi na umvike Haruni koti, joho la kisibau na kisibau chenyewe pamoja na kile kifuko cha kifuani. Mfungie hicho kisibau kwa ule mshipi wa kiunoni uliosukwa kwa ustadi. 6 cWeka kilemba kichwani mwake na kuweka taji takatifu ishikamane na hicho kilemba. 7 dChukua yale mafuta ya upako umimine juu ya kichwa chake. 8 eWalete wanawe na uwavike makoti, 9 fpia uwavike zile tepe za kichwani. Ndipo uwafunge Haruni na wanawe mishipi. Ukuhani ni wao kwa agizo la kudumu. Kwa njia hii utamweka wakfu Haruni na wanawe.

Copyright information for SwhKC